Share news tips with us here at Hivisasa

Wanasiasa Nyamira wameonywa dhidi ya kujihusisha na siasa zakuwadaganya wakazi.

Akizungumza siku ya Jumanne, kwenye hafla yakuadhimisha siku ya mashujaa kule Nyamaiya, Gavana wa kaunti hiyo John Nyagarama aliwaomba wanasiasa kutafuta njia mbadala zakupiga siasa zao badala ya kueneza siasa potovu ambazo haziwezi saidia kustawisha maendeleo.

“Nawaomba wanasiasa humu Nyamira kutafuta njia mbadala zakufanya siasa zao badala yakueneza siasa zisizo weza kustawisha maendeleo ya kaunti hii. Nawasihi wananchi kupuuza wanasiasa wa tabia kama hizo," alisema Nyagarama.

Aliongeza, "Siasa potovu zinazo enezwa na baadhi ya viongozi ni mojawapo ya vizingiti vya maendeleo na nawapa changamoto viongozi hao kushiriki kwenye miradi ya maendeleo kwa kuwa hayo ndiyo matarajio ya wapiga kura."

Gavana Nyagarama aidha alisema kuwa amejitolea kuhakikisha kuwa miradi mbalimbali ya maendeleo inafanikiwa chini ya uongozi wake.

"Mimi binafsi nimejitolea kuhakikisha kuwa miradi ya maendeleo inafanikiwa na iwapo wananchi wataamua kuningoa mamlakani hata baada yakuwajengea barabara, kujenga shule za chekechea, kujenga hospitali na kuweka madawa pamoja na mashine kwenye hospitali hizo na zahanati zetu, basi nitaondoka mamlakani bila ubishi," alisema Nyagarama.