Viongozi Pwani wamejitokeza na kupongeza uamuzi wa mahakama ya Kimataifa ya uhalifu wa Kivita ICC kuhusu uamuzi uliyotoa kuhusu kesi iliyokuwa ikimkabiliwa Naibu Rais William Ruto na mwanahabari Joshua Sang.

Share news tips with us here at Hivisasa

Wakizungumza mjini Mombasa siku ya Jumapili, viongozi hao wakiongozwa na mbunge wa Kilifi Kaskazini Gideon Mung’aro walisema kuwa mahakama hiyo ilichukua uamuzi wa busara na wenye hekimu katika kusitisha kesi hiyo kwani Wakenya walikuwa wameipokea katika mtizamo wa kisiasa.

Mung’aro alisema kuwa joto la kisiasa nchini limekuwa tayari limepanda na jinsi Wakenya wanavyokaribia uchuguzi mkuu huenda kukazuka vurugu lakini uamuzi huo umepunguza kwa kiasi kikubwa joto la kisiasa na tumaini lao kubwa Kenya itakuwa nchi ya amani.

Kiongozi huyo wa kisiasa aidha aliwataka wakaazi wa Pwani na Wakenya kwa jumla kuhakikisha kuwa wanadumisha amani na kutangamana kama jamii moja ili kuondoa chuki, ukabila na maswala ya kidini ambayo huwatenganisha Wakenya.

“Sisi kama viongozi wa Pwani tunapongeza moja kwa moja uamuzi uliyotolewa na mahakama ya ICC dhidi ya kesi amabyo ilikuwa ikimkabilia kiongozi wetu naibu Rais William Ruto na aliyekuwa mwanahabari Joshua Sang na tunatumaini kubwa kuwa Wakenya watazidi kudumisha amani na kuishi kwa undugu,” alisema Mung’aro.

Kauli ya Mung’aro iliungwa mkono na mbunge wa Kilifi Kusini Mustafa Idd alidai kuwa uhasama wa chuki za kisiasa sasa zitasaulika na wakenya kudumisha zaidi amani huku akisema kuwa wtahakikisha wameungana na viongozi wengine nchi kuhudhuria maombi ya amani mjini Nakuru siku ya Jumamosi.