Viongozi mbalimbali wa dini wamepongeza uteuzi wa Askofu Jackson Ole Sapit wa Kanisa la Kianglikana Jimbo la Kericho, kama askofu mkuu mpya wa kanisa hilo nchini.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akizinhumza na mwandishi huyu siku ya Ijumaa katika mahojiano kupitia njia ya simu, askofu wa Kanisa la Kianglikana jimbo la Mombasa, Askofu Julius Kalu, alisema kuwa Ole Sapit ni kiongozi anayependa kuwaunganisha waumini na Wakenya, hivyo basi ana imani kuwa kanisa hilo litaendelea kueneza amani.

“Tunapongeza uteuzi wa Askofu Ole Sapit na tutafanya kazi naye kama kiongozi wetu ili kuhakikisha kuwa kanisa linatumikia Mungu vyema, na kuwaunganisha waunimi pamoja,” alisema Askofu Kalu.

Askofu Ole Sapit atachukua nafasi ya Askofu Mkuu wa sasa Dkt Eliud Wabukhala anayetarajiwa kustaafu mwezi ujao.

Askofu Ole Sapit aliye na umri wa miaka 51 ataapishwa rasmi kuchukua uongozi wa kanisa hilo tarehe tatu mwezi Julai, katika hafla itakayoandaliwa katika Kanisa la All Saints Cathedral, jijini Nairobi.