Maseneta wote ambao wameweka wazi azma yao ya kuwania kiti cha ugavana katika gatuzi zao wameombwa kujiondoa katika kamati za seneti zinazowahoji magavana kuhusu jinsi wanavyoendesha shugli za kaunti.

Share news tips with us here at Hivisasa

Hii ni baada ya vita kali baina ya magavana na maseneta hao kushuhudiwa katika vikao vya seneti ambazo magavana hao huagizwa kufika

Katika kaunti ya Mombasa viongozi wa mrengo ya Jubilee wakiongozwa na Amina Abdalla wamemkashifu seneta Hassan Omar kwa kumuagiza gavana wa kaunti ya Mombasa Hassan Joho kufika mbele ya kamati ya seneti ili kueleza jinsi serikali ya kaunti imetumia fedha walizotengewa.

Aidha Amina Abdalla ambaye ni mshirikishi wa mrengo huo katika kaunti ya Mombasa amesema kuwa Seneta  ashaweka wazi azma yake ya kuwania kiti cha ugavana na hana mamlaka yoyote ya kumtaka gavana huyo kuhojiwa.