Share news tips with us here at Hivisasa

Viongozi wa chama cha Kanu katika kaunti ya Uasin Gishu wamekashifu matamshi ya Naibu wa Rais William Ruto aliyosema wikendi akiwa Kericho.

Kulingana nao, Ruto alinaswa akisema kuwa kiongozi wa chama cha Kanu, Gideon Moi, hajapashwa tohara. 

"Naibu wa rais anatumia njia mbaya kutafuta kura, anatakiwa kuacha njia hizo," alisema Chepsiror. 

Wakizungumza na wanahabari katika hoteli ya Sirikwa, mwenyekiti wa Kanu Uasin Gishu, David Chepsiror alisema kuwa naibu wa rais anatakiwa kuacha siasa ya uchochezi na matusi. 

"Kuita vyama vingine maiti au vyama vya wajinga ni hatia sana," alikariri Chepsiror.

 Aidha, viongozi hao wamemtaka Ruto kuomba Wakenya msamaha kwa matamshi yake. 

 "Ruto aombe msamaha kwa chama cha Kanu, viongozi wake, na wananchi kwa jumla," alisema Chepsiror.