Share news tips with us here at Hivisasa

Kutokana na kukithiri kwa visa vya uhalifu katika Kaunti ya Mombasa, viongozi wa kisiasa na wale wakidini wameunga ili kubuni mbinu mbadala za kudhibiti usalama.

Wakiongozwa na Mwakilishi wa Wadi ya Jomvu katika eneo bunge la Jomvu, Kaunti ya Mombasa, Karisa Nzai, viongozi hao walisema kwamba kwa ushirikiano baina ya wakazi, viongozi wa kisiasa na wale wa kidini, eneo la Jumvu litaimarika kiusalama.

Akiongea katika mkutano wa amani uliyohudhuriwa na zaidi ya maimam 50 wa dini ya kiislam katika eneo la Jomvu siku ya Alhamisi, Nzai alisema kwamba maafisa wa usalama wamejitolea kikamilifu kukabiliana na wahalifu.

“Maafisa wa usalama wamejitolea kikamilifu kukabilina na wahalifu na kusitisha kukithiri kwa visa vya kihalifu na iwapo viongozi wa kidini na wakazi tutashirikiana na maafisa wetu wa usalama, basi eneo hili litakuwa salama,” alisema Nzai.

Aidha, aliihimiza jamii ya kiislam kujitokeza na kupiga vita uhalifu kwani mara nyingi baadhi ya wafuasi wa dini hiyo huitumia dini ya kiislam kinyume na mwongozo wa dini hiyo na jinsi inavyoangazia.

“Ningependa kuwahimizwa ndugu zangu wa kiislam tafadhali tushirikiane katika kusitisha kuenea kwa visa vya kihalifu ili kuona kwamba wale vijana walijiunga na makundi haramu tunawanasua na kuwapa ajira za kujikimu kimaisha. Tafadhili tusidanganywe na kuitumia dini vibay kwani sote na wakenya na lazima tushirikiane,” alisema Nzai.

Viongzo hao wameahindi kuzuru mashinani na kuihamasisha jamii jinsi ya kushirikiana na maafisa wa usalama pamoja na viongozi katika kutoa habari muhimu kuhusu washukiwa wa uhalifu ili watiwe nguvuni.