Baadhi ya viongozi wa kidini kwenye kaunti ya Nakuru wamepinga hatua ya kenya kujiondoa kwenye makataba wa Roma uliounda mahakama ya kimataifa ya jinai ICC.
Wakizungumaa na wanahabari jumanne hii, viongozi hao wakiongozwa na askofu wa dhehebu la talents revival churches kamuri muya wamesema hatua ya kenya kujiondoa kwenye mkataba wa roma itapelekea baadhi ya viongozi kutoadhibiwa hata baada ya kuhusika katika ukiukaji wa haki za kibinadam katika siku za usoni.
Kamuri ametaja mahakama ya kimataifa ya jinai icc kama mtihani kwa kenya akiongeza kuwa mahakama hiyo ilitumika kama njia ya kuwafanya wanasiasa kuchukua tahadhari huku wakijibidiisha kupata viti vya uongozi.
Ingawa amekiri kuwa taifa la kenya limeanza safari ya kutafuta uponyaji wa kitaifa na kusameheana, amesema kuna haja ya kuhakikisha wanasiasa wanazuiwa dhidi ya kuwachchea watu kueneza ghasia.
Wakati huo huo, amesisitiza kuwa mkondo ambao umechukuliwa na mrengo wa uypinzani kutafuta mageuzi na haswaa yale ya walio katika tume ya uchaguzi na mipaka iebc haufai huku akitaka mrengo huo kutii sheria ili kuzuia tukiosawia na lililoshuhudiwa jumatatu hii.
Kamuri ambaye pia ni balozi wa amani katika kaunti ya nakuru aidha ameangazia hatua ya rais uhuru kenyatta na naibu wake kufanya maombi ya shukrani mjininakuru hivi masajuzi akisema hatua hiyo ni ishara ifaayo haswaa kutoka kwa uongozi wa taifa hili.