Viongozi wa kidini wamekashifu makundi ya kinamama katika Kaunti ya Mombasa kwa kuzozana hadharani wakati wa sherehe za kitaifa.
Haya yanajiri baada ya wafuasi wa Gavana Hassan Joho na Mbunge wa Nyali Hezron Awiti kuzua vurugu wakati wa sherehe za Jamuhuri katika uwanja wa Tononoka.
Askofu mkuu wa kanisa katoliki jimbo la Mombasa Martini Kivuva amesema hatua hiyo haikuwa na twasira nzuri katika ukuzaji wa maadili ya watoto katika jamii.
Akiongea mjini Mombasa siku ya Jumatano, Askofu Kivuva aliikashifu hali hiyo huku akiitaja kama inayolenga kuwapotosha watoto kimaadili.
“Ningependa kuwaomba wazazi kuonyesha mfano mwema katika matendo wanayoyafanya ili watoto wao waweze kuiga tabia nzuri,” alisema Kivuva.