Hatua ya wizara ya maswala ya ndani nchini ya kupunga walinzi wa viongozi wa kisiasa imetajwa kuwa jambo la busara kwani wananchi watapata usalama dhabiti.
Katibu mtendaji wa baraza la maimamu na wahubiri humu nchini CIPK, Sheikh Mohamed Khalifa alisema kuwa viongozi wa kisiasa nchini wamekuwa na desturi ya kuwa na walinzi wengi huku wananchi wakisalia kulalamikia usalama duni.
Akizungumza na mwanahabari huyu mjini Mombasa siku ya Jumanne, Sheikh Khalifa alisema kuwa walinzi hao waliyopunguzwa kutoka kwa viongozi watasaidia katika kuwalinda wananchi sambamba na kuboresha usalama wa wanaishi walio katika maeneo yaliyokosa usalama kwani wananchi sasa wataishi bila hofu.
"Tunapongeza hatua ya serikali kuwapunguzia viongozi wetu wa kisiasa walinzi kwa sababu walinzi hao sasa watakuwa wanalinda wananchi na hatua hiyo itaboresha usalama wa wananchi na kuishi bila hofu yoyote kulinza walinzi kumi wamlinde mtu mmoja huku mlinzi mmoja alinde watu 400, hilo sio jambo jema,'' alisema Sheikh Khalifa.
Kiongozi huyo wa kidini aidha amesema kuwa iwapo viongozi watakuwa na mienendo mizuri na kuepukana na ukabila, ufisadi na maneno ya chuki basi wataishi bila hofu ya kuandamwa na wahasidi wao.