Viongozi wa kidini katika kaunti ya Nakuru wameonekana kuunga mkono hatua ya serikali ya kutaka kufunga kambi za wakimbizi hapa nchini.
Akiangazia swala la Kenya kufunga kambi za wakimbizi za Daadab ba Kakuma hapa nchini, askofu wa dhehebu la Independent Church Naftali Thuku hata hivyo ametaka wakimbizi walio katika kambi za wakimbizi hapa nchini kupewa muda wa kutosha kujitayarisha kabla ya kuondolewa katika kambi hizo.
Aidha, ametaka taratibu zifaazo zifwate katika kuwaondoa wakimbizi hao katika kambi hizo.
‘ Kwa kweli ni vizuri kama bi kufunga lakini kufwate njia sawasawa. Wasiondolewe mbio mbio. Wapewe nafasi ya kutosha ya kujiandaa na kuondoka. Ni vizuri kama wanarudishwa , utaratibu unaofaa ufwate.
Ni vyema kukariri hapa kuwa matamshi haya ni kinyume na yale ambayo yamekuwa yakitolewa na watetezi wa haki za kibinadam ambao wamekuwa wakikosoa serikali kwa uamuzi wa kutaka kufunga kambi hizo.
Shirika la Kenya National Commission on Human Rights (KNCHR) Jumatatu hii mjini Nakuru kupitia kwa naibu kamishna wa tume hiyo George Morara ilikariri kuwa hatua hiyo ya serikali itawadhuru wakimbizi na kuwaweka katika hali ya hatari.