Baraza la muungano wa madhehebu mbalimbali humu nchini maarufu Inter-religious Council limeshtumu vikali matamshi ya baadhi ya wanasiasa ambapo huenda yakayumbisha amani na utulivu.

Share news tips with us here at Hivisasa

Ronald Sanros Sunguti kutoka baraza hilo katika mahojiano na wanahabari mjini Nakuru Jumamosi, alisema kuwa ni jambo la busara kwa wanasissa kujali matamshi yao kwani yanaweza kubomoa au kujenga taifa.

"Ningependa kuwaomba wanasiasa watumie muda huu kujali sana matamshi yao hasa tunapokaribia uchaguzi mkuu,"alisema Sunguti.

Na huku taifa likiwakumbuka walioathiriwa na mkasa wa chuo kikuu cha Garissa, Sunguti alisema kuwa wakati ni sasa kwa wakristo na waislamu kuzidi kushirikiana ili kuaibisha adui.

Aliongeza kuwa kama baraza la madhehebu mbalimbali, watazidi kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa amani.

Ni vyema kuashiria hapa kwamba baraza la madhehebu limekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha umma kuhusu umuhimu wa amani.