Mkurugenzi mkuu wa Chama cha Watalii nchini yaani ‘Kenya-Coast Tourist Association’, Bi Milicent Adhiambo amewataka viongozi wa kisiasa Pwani kuhakikisha kuwa wanafanya kampeni zao kwa njia mwafaka ili kuzuia kusambaratisha sekta ya utalii nchini.
Akizungumza mjini Mombasa, Bi Milicent amesema kuwa jinsi viongozi wa kisiasa wanavyofanya kampeni zao za kujipigia debe kwa uchaguzi mkuu ujao wanazitekeleza kwa njia zisizofaa na huenda zikasababisha uhasama na kuvurugu usalama.
Amesema kuwa iwapo eneo la Pwani itakuwa na usalama duni basi sekta ya utalii itasambaratika na kuchangia kushuka kwa uchumi wa nchi kwani sekta hiyo tayari imeanza kuimarika kufuatia juhudi za wadau wa sekta hiyo.
"Itakuwa vyema iwapo viongozi wetu wa kisiasa ambayo wamejitokeza kufanya kampeni zao watazifanywa kwa njia ya amani na kuwaunganisha Wapwani ili kuzuia kushughudiwa kwa vuurugu la kusababisha kusambaratika kwa sekta ya utalii," alisema Milicent siku ya Jumanne mjini Mombasa baada ya kutokana na wadau wa sekta ya utalii.
Bi Milicent amewataka viongozi wa kisiasa Pwani kuhakikisha kuwa wanafanya kampeni zao kwa amani na kuwaunganisha Wakenya ili kuzuia kuzuka kwa siasa za chuki, akisema kuwa siasa za amani ndizo muhimu kwa taifa hili lenye kuzingatia demokrasia.