Viongozi wa Kiislamu wa vyama vya SUPKEM na CIPK wammpongeza Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto kwa kuongoza nchi katika maombi ya kusameheana katika uwanja wa Afraha siku ya Jumamosi.
Aidha, viongozi hao wametoa wito kwa rais na naibu wake kuhakikisha waathiriwa waliosalia wamefidiwa ipasavyo ili waweze kurudia maisha yao ya hapo awali kabla ya vita vya baada ya uchaguzi wa mwaka 2007/2008
Wakiongozwa na Sheikh Abubakar Bini, viongozi hao walisema kuwa hatua hiyo itaimarisha juhudi za maridhiano halisi miongoni mwa Wakenya haswa baada ya kesi za ICC kutupiliwa mbali.
Kwa upande wake, Sheikh Abdikadir Mohammad wa SUPKEM ameitaka serikali kuwahudumia Wakenya vilivyo baada ya kutupiliwa mbali kwa kesi hizo.
Aidha, sheikh huyo alitoa wito wa kusamehewa na kurejeshwa nyumbani vijana walioshawishika kutoa ushahidi wa uwongo.