Katibu mkuu wa KNUT tawi la kilidini .Dan Aloo .[ mediamaxnetwork.co.ke]Muungano wa chama cha walimu nchini KNUT tawi la mombasa unataka wadau wote wa elimu washirikishwe katika mchakato wa kusahihisha upya mitihani ya kitaifa ya kidato cha nne KCSE.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wakiongozwa na katibu mkuu wa KNUT tawi la kilidini Dan Aloo maafisa hao wanasema ni vigumu kusahihisha mitihani ya kidato cha nne kwa mda mfupi uliotumika kusahihisha mitihani hiyo.

“Ni jambo la kushangaza kusahihisha mtihani huo kwa mda mfupi, lazima kuna filifinyange ilifanyika hapo”,alisema Aloo.

Amesema hana imani na uhalali wa matokeo hayo kama yalivyotangazwa hivi majuzi na waziri wa elimu Fred Matiang’I.

“Sina imani kabsa na jinsi mtihani huo ulivyosahihishwa na baraza la mitihani”,alisema Aloo.

Akiongea na waandishi wa habari siku ya Ijumaa, jijini mombasa Aloo amesema ipo haja ya kurejelea zoezi hilo na kumtaka waziri Matiang’I kushirikiana na wadau wengine katika sekta ya elimu ili kuyatafutia ufumbuzi masuala tata yanayoathiri sekta hiyo.

Is there a newsworthy accident, incident or event happening in Mombasa County that you want Hivisasa to cover? Tell us what is happening by Joining this group, and have it published.*https://chat.whatsapp.com/5K1mGBnRVB46Mixhdh5caF