Share news tips with us here at Hivisasa

Viongozi wa mrengo Cord katika kaunti ya Kwale wamesema Shutuma zinazo mkabili gavana wa Mombasa Hassan joho hazina ukweli wowote.

Wakiongea na wanahabari kwa njia ya mahojiano uko Kwale, viongozi hao wamesema kuwa vitendo vinavyofayinyiwa gavana Joho ni vya kisiasa na pia ni vya kudhulumu viongozi wa Cord.

Haya yamejiri baada ya gavana huyo wa Mombasa kupokunywa walinzi wake kwa kile kinachodaiwa kuenda kuongeza viwango vyao vya elimu, huku pia akitakiwa kuwasilisha silaha zake za ulinzi.

Viongozi hao wametaja kuwa mfumo wa serikali kutumia chama kimoja katika kutawa ulipitwa na wakati na ni wa kikoloni.

Hata hivyo,  wameitaka serikali ya Jubilee kukoma kuwaangaisha viongozi wa Cord hususani wa Pwani.