Baadhi ya viongozi wakisiasa kaunti ya Mombasa wameunga mkono hatua ya spika wa bunge la kitaifa Justine Muturi ya kumchukulia hatua za kinidhamu mbunge wa Ugunja Opiyo Wandayi aliyelenga kutatiza hotuba ya rais Uhuru Kenyatta kwa wananchi bungeni humo juma lililopita.
Akizungumza na wanahabari pembezoni mwa bunge la kaunti hiyo, mjumbe Saad Faraj amesema hatua hiyo itakuwa funzo kubwa kwa viongozi walio na tabia hizo.
Aidha amesisitiza kuheshimiwa kwa rais wa taifa Uhuru Kenyatta na sheria lazima ufuate mkondo wake.
Faraj amesema hatua ya mrengo wa upinzani kutaka kufikisha lalama za mbunge huyo mahakamani sio mwafaka akidai mbunge huyo amehukumiwa na sheria wanazopitisha wenyewe bungeni humo.