Chama cha TNA tawi la Mombasa kimepinga vikali maandamano yaliyotekelezwa siku ya Jumatatu jijini Mombasa na kusema kuwa hatua hiyo italeta ukosefu wa usalama.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mwenyekiti wa chama cha TNA tawi la Mombasa Mohammed Salim , amedai kuwa hakukuwa na haja ya maandamano hayo katika kaunti ya Mombasa kwa kuwa makao makuu ya IEBC yanapatikana jijini Nairobi.

Aidha, siku ya Jumannne, aliongeza kuwa iwapo maandamano hayo yatazidi fanywa jijini Mombasa basi yatatiza utalii wa eneo hilo.

Pia wamentaka gavana Joho kuwa mstari wa mbele kuongoza maandamano dhidi ya masuala muhimu kama kukithiri kwa ulanguzi wa dawa za kulevya miongoni mwa masuala mengine yanayoathiri wakaazi wa kaunti ya Mombasa.