Wanasiasa wa vyama vya Jubilee na Wiper Kaunti ya Kwale wamewakosoa viongozi wa upinzani kwa kumkosea heshima Rais Uhuru Kenyatta.
Mhirikishi wa chama cha Jubilee Kwale Mshenga Vuya Ruga, amemshutumu Gavana wa Mombasa Hassan Joho kwa kumzomea Rais Kenyatta hadharani.
Ruga alisema kuwa hataua hiyo inahujumu kiongozi wa taifa.
Aidha, amewataka viongozi wa upinzani kuepuka kutumia lugha chafu na kumkejeli rais wanapokuwa majukwaani.
Ruga pia alipuzilia mbali madai kuwa hatua ya serikali kuwapokonya Gavana Hassan Joho na mwenzake wa Kilifi Amason Kingi walinzi wao ilichangiwa kisiasa.
Kwa upande wake, katibu wa chama cha Wiper eneo la Diani Katiba Mkungu amewataka viongozi wa upinzani kuheshimu rais pamoja na viongozi wengine.
Amemtaka Joho kutumia njia mwafaka ya kuwasilisha matatizo yake kwa serikali badala ya kumkemea kiongozi wa taifa hadharani.