Wawakilishi wa Wadi katika jimbo la Nakuru wameikaribisha hatua ya ulipaji wa ushuru kwa njia ya elektroniki [automotive revenue collection] hasa ile ya malipo ya kuegeza magari wakisema kuwa hatua hiyo itatatua swala la ufisadi na kuliongozea jimbo hilo mapato na hivyo kuimarisha uchumi wake.
Wakiongozwa na Samwel Tanui na ambaye ni naibu wa spika katika bunge la jimbo hilo wawakilishi hao wameipongeza hatua hiyo huku wakiwataka wananchi kuikumbatia kwa misingi kuwa hakutakuwepo na utumizi wa risiti. Tanui amehoji kuwa hatua hii itapunguza visa vya marisiti ya uongo ambavyo vinatekelezwa na baadhi ya wafanyikazi na kisa kuepa na helazinazonuiwa kuimarisha kiwango cha jimbo.
Amedai kuwa jimbo la Nakuru limekuwa likipoteza idadi kubwa ya pesa kwa kutumia mbinu hiyo ya awali ya kulipa na kupokea risiti akiongeza kuwa ni hatua itakayohakikisha kuwa kila mwananchi anayeegeza gari lake amelipa bila upendeleo kwa misingi kuwa zitakuwa zinaashiria kwa mashine papo hapo.