Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Viongozi wanaoshirikiana na vijana kutekeleza visa vya kihalifu katika kaunti ya Mombasa, sasa chuma chao kimotoni baada ya idara ya usalama kaunti hiyo kutangaza kukabiliana nao.

Kamishna wa kaunti ya Mombasa Nelson Marwa,alisema kuwa kuna baadhi ya viongozi wa kisiasa katika kaunti hiyo wanaowafadhili vijana kujiunga na makundi ya kihalifu na kuwanyanyasa wakazi wasio kuwa na hatia na kusababisha hofu miongoni mwao.

Akizungumza mjini Mombasa siku ya Jumanne katika kikao na wanahabari, Marwa alisema kuwa iwapo viongozi hao hawatashirikiana na jamii kubadilisha mienendo ya vijana hao basi maafisa wa usalama wataanza na viongozi hao kuwatia nguvuni kisha kuwakabili kijana hao.

Alisema kuwa serikali iko macho kuhakikisha kuwa usalama unaimarisha huku akiyaonya makundi ya kihalifu hasa Wakali Kwanza na Wakali Wao kusalimu amri ya maafisa hao kabla ya kukabiliwa kikamilifu.

"Serikali iko macho kuhakikisha kuwa usalama unaimarishwa na wale viongozi wanashirikiana na vijana kufanya uhalifu tutanza na hao kuwakabili na hakuna huruma kwa sababu jukumu la kiongozi ni kuwaongoza vijana vizuri sio kusababisha hofu kwa jamii," alisema Marwa. 

Kamisha huyo wa kaunti ya Mombasa, hata hivyo amewahakikishia wakazi wa kaunti hiyo usalama dhabati huku akiwataka kushirikiana na maafisa wa usalama katika kutoa habari muhimu kuhusu washukiwa wa ugaidi na uhalifu ili kutiwa nguvuni.