Share news tips with us here at Hivisasa

Viongozi akina mama katika eneo la Pwani wamewashutumu baadhi ya wabunge kwa kutounga mswaada wa usawa wa jinsia uliokosa kupitishwa bungeni wiki iliyopita.

Wakizugumza mjini Malindi, mwakilishi wa akina mama katika Kaunti ya Mombasa Bi Mishi Mboko na mwenzake wa Kilifi Aisha Jumwa, waliwasuta wabunge wa mrengo wa Jubilee ambao walikosa kutumia wingi wao bungeni kupitisha msaada huo wa jinsia.

Mwakilishi wa wanawake Kaunti ya Kilifi Bi Jumwa alisema kuwa akina mama wanaingia bungeni kupitia njia ya kupigiwa kura mashinani.

“Ni jambo la kusikitisha na la aibu kuwa bado mwanamke hajapata haki yake kama inavyostahili katika karne ya 21,” alisema Jumwa.