Wanasiasa nchini wameonywa dhidi ya kutoa matamshi ya chuki hasa wakati huu ambapo taifa linajiandaa kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2017.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akizungumza siku ya Alhamisi mjini Mombasa, Naibu Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini CA kanda ya Pwani, Joseph Kamunge, aliwataka wanasiasa kujihusisha pakubwa katika kuunganisha Wakenya.

Kamunge alisema kuwa baadhi ya wanasiasa nchini wanaendeleza siasa za kuwagawanya Wakenya pasi kujali katiba inavyosema.

“Ningependa kuwaonya wananchi dhidi ya kuwafuata viongozi kama hao wasiokuwa na malengo ya kimaendeleo,” alisema Kamunge.

Kauli yake inajiri baada ya kushudiwa joto la kisiasa nchini kutoka kwa wanasiasa wa mirengo yote nchini.