Aliyekuwa mbunge wa Subukia Koigi Wa Wamwere, amesema uamuzi wa mahakama ya kimataifa ICC huenda ukawapa viongozi nafasi ya kubadilisha katiba ili kuwaruhusu kuongeza muda wao madarakani.
Koigi aliye pia mchanganuzi wa maswala ya Kisiasa amesema kuwa kesi zilizokuwa zikiwakabili naibu wa rais William Ruto na Joshua Sang zinaweza zikarudiwa ikiwa ushaidi wa kutosha utakuwepo.
Akizungumza Jumamosi katika mahojiano na kituo cha redio cha Sauti ya Mwananchi, Koigi alisema hatua ya Muungano wa Umoja wa Afrika AU, kushinikiza kujiondoa katika mahakama ya ICC, inadhihirisha jinsi viongozi hao walivyojitayarisha kuparamia mamlaka.
“Sikubaliani na uamuzi wa mahakama hiyo kabisa kwa sababu inafungua mianya kwa viongozi madikteta kujiongezea muda wa uongozi na kukiuka sheria za nchi,” alisema Koigi.
Alisema mbinu ya icc kuwasubiri viongozi wanapomaiza muda wao wa uongozi kisha kuwafungulia mashtaka ni mbinu nzuri japo alipendekeza kuwa mahakama haingefichua kuwa huenda wakarudia kesi iliyoamuliwa tayari kwa sababu viongozi ambao wamekuwa wakitafutwa kama rais wa Sudan Omar El Bashir, watasaia madarakani kwa kuogopa kushikwa na mahakama hayo.