Baadhi ya viongozi nchini wanakabiliwa na athari ya kupoteza viti vyao iwapo hawataweka mikakati mwafaka kabla ya uchaguzi wa mwaka ujao.
Wengi wa wale ambao wanakabiliwa na athari hiyo ni pamoja na magavana, maseneta, wabunge na wawakilishi wadi wengi nchini.
Athari hizi zinatokana na matamshi na vitendo vya wanasiasa hawa. Kwa mfano, huenda mbunge wa Kitutu Masaba Timothy Bosire akapoteza kiti chake kutokana na matamshi yake katika kumbi na mikutano mbalimbali ukiwemo ule wa mazishi ya babake Walter Nyambati, aliyekuwa mbunge eneo hilo.
Bosire pia alikaidi amri ya kusimama bungeni kuwakumbuka wanajeshi walioaga Somalia.
Gavana wa Nyamira John Nyagarama naye ni mfano mwingine. Serikali yake imekumbwa na visa vingi vya ufisadi ambavyo yeye na serikali yake wameshindwa kudhibiti na kuvielezea.
Viongozi wengine ni Evans Kidero, Hassan Omar, Richard Tong'i na wengineo. Viongozi hawa wanaweza kukwepa athari hii iwapo wataweka mikakati mwafaka ili kuwarai wananchi.