Seneta wa Mombasa Hassan Omar amesema ipo haja ya viongozi wa muungano wa Cord kukutana ili kuondoa kujadili mbinu muafaka kuondoa tashwishwi kuhusu mgombeaji wa uraisi katika muungano huo wa uchaguzi wa 2017.
Omar amesema kulingana na mkataba huo, aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga alikuwa amepewa nafasi ya kuongoza kwa mda wa miaka mitano kama raisi lakini ndoto haikutimia.
Aidha alisema kuwa makubaliano hayo yalikuwa ni fursa ya Kalonzo Musyoka sasa kuwania uraisi kupitia tikiti hiyo chama cha Cord.
Amedokeza kuwa mjadala unaoendelea ni fursa ya kidemokrasia ambayo inakubaliwa lakini viongozi katika muungano huwo sharti wawe makini.
Hata hivyo amewaomba viongozi wenzake kuwa na uvumulivu na umoja iwe kipao mbele kwenye muungano huwo kudumu na kuleta maendeleo kwa Wakenya kulingana na manifesto yao.