Utafiti uliofanywa hivi karibuni umeonyesha kuwa visa vya ugonjwa wa malaria umeongezeka katika kaunti za kanda ya Pwani licha ya visa hivyo kupungua katika sehemu zingine za nchi.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Utafiti huo uliofanywa na taasisi ya kitaifa ya kudhibiti ugonjwa wa malaria katika wizara ya afya nchini pia imeripoti kuwa ongezeko la ugonjwa huo katika kanda ya Pwani umeongezeka kutoka asilimia 4 hadi asilimia 8.

Akisoma ripoti hiyo siku ya Jumatano, kaimu mtendaji katika wizara ya afya Nicholas Muraguri alisema kuwa idadi ya visa hivyo vya malaria vimepungua nchini kutoka asilimia 11 mwaka wa 2010 hadi asilimia 8 mwaka huu.

Wizara hiyo sasa imetoa wito kwa serikali ya kaunti ya Mombasa kushirikiana na maafisa katika wizara hiyo ili kuhakikisha kuwa visa vya ugonjwa wa malaria ambayo iko miongoni mwa magonjwa yanayoua watu wengi duniani vimepungua.