Mwenyekiti wa bodi ya elimu kaunti ya Kisii Henry Onderi amefutilia mbali maoni ya watu wanaosema shule za Kisii zinakumbwa na mikasa ya moto kufuatia nguvu za kishetani
Alikuwa akiongea katika shule ya upili ya wavulana ya Nyachwa iliyoko wadi ya Kisii ya kati kaunti ya Kisii, wakati wa kuwazawadi wanafunzi waliofanya mtihani vyema wa kidato cha nne mwaka jana.
Onderi alisema kuwa kinachosababisha mikasa ya moto katika mashule ni kutounganishwa vizuri kwa nyaya za stima katika mashule, wanafunzi kuweka simu zao kwa moto ambazo hazitakiwi kwa shule, wanafunzi kuchemsha maji ya kuoga na hata wanafunzi kufanyi hivyo maksudi wakilalamikia jambo flani.
Wakati huo huo, mwenyekiti huyo aliwaomba wasimamizi wote wa shule mbalimbali; hasa zilizochomeka kuwa watulivu huku uchungunzi ukiendelea kufanywa kuhusiana na mikasa hiyo.
“Nawaomba wanafunzi mkiona moto umetokea msijaribu kuingia kwa bweni hata kwa madarasa kwamba mnahitaji kusaidia vitu zenu, la hasha, maana mnaeza kumbwa na moto na kuchomeka,” alidai Onderi.
Katika kaunti ya Kisii, zaidi ya shule 5 zimekumbwa na mkasa wa moto, zikiwemo shule ya wavulana ya Cardinal Otunga Mosocho, St. Peters Suneka, shule ya wasichana ya St. Angela, St. Peters Nyamesocho, Mochengo na Sister Michael.
Mwenyekiti huyo aliwahakikishia wakazi wa Kisii kuwa uchungunzi unaendelea kufanywa dhidi ya mikasa ya moto na suluhu litapatikana karibuni.