Ripoti kutoka kwa vuguvugu la walimu linalojiita Kenya Network of Beacon Teachers inaonyesha kuwa kaunti za kanda ya Pwani zinaongoza katika visa vya ukatili dhidi ya wanafunzi shuleni.

Share news tips with us here at Hivisasa

Ripoti hiyo pia inaonyesha kuwa Kaunti ya Kilifi ndio inayongoza kwa takribana visa 180 kati ya mwaka wa 2015 na 2016 ikifuatiwa na kaunti ya Kwale, Tana River, Taita Taveta, Lamu na Kaunti ya Mombasa.

Afisa mkuu wa vuguvugu hilo Joan Nguzi, alitaja viwango vya umasikini katika kaunti hizo kama jambo ambalo linachangia sana ukatili dhidi ya wanafunzi.

Visa vilivyoripotiwa ni pamoja na visa vya watoto kuadhibiwa kupita kiasi cha kawaida na visa vya wanafunzi kunyanyaswa kimapenzi.

Ripoti hiyo ilisomwa kwenye mkutano na walimu kutoka kaunti za Pwani siku ya Jumapili mjini Mombasa.