Visa vya watoto kujihusisha na biashara ya ukahaba vimeripotiwa kuongezeka katika kaunti ndogo ya lungalunga na horohoro kwenye mpaka wa Kenya na Tanzania.

Share news tips with us here at Hivisasa

Mashirika ya kijamii yamejitokeza kupinga vikali hali hiyo inayosemekana kusababishwa na jamii kutojukumika ipasavyo ili kutoa malezi mema kwa watoto hao.

Madereva wa malori ya mizigo, wenye vilabu na mabanda ya video pamoja na wahudumu wa bodaboda wametajwa kuwa mstari wa mbele kuhusika kwenye visa hivyo ambavyo vimechangia idadi ya mimba za mapema kuongezeka katika eneo hilo.

Mbunge wa watoto katika eneo hilo Ndinda Kyalo amemtaka OCS wa eneo hilo kupeleka kesi hizo kortini pindi zinaporipotiwa na waathiriwa wa visa hivyo.

Afisa wa polisi anayelinda haki za watoto Lawrence, amesema kuwa wao hupokea kesi mbili hadi tano kwa juma.

Afisa huyo ameonya kuwa yeyote atakayepatikana akitekeleza dhulma hizo atakabiliwa na sheria kwa sababau vitendo hivyo vinapofanyika humnyima mtoto haki yake ya kimsingi.

Haya yanajiri baada ya maandamano ya kupinga dhulma hizo yaliyofanyika huko lungalunga kwa ufadhili wa shirika la Strengthening Community Partnership and Empowerment (SCOPE).