Siku chache baada ya kutangaza kuwa mja mzito na kutarajia mototo wa sita akiwa katika hospitali moja nchini Afrika Kusini, msanii wa kikee kutoka hapa nchini Akothee ameendelea kuwatamausha wengi baada ya kuonyesha  gari la kifahari aina ya Ferrari, alilodai kuzawadi na mpenzi wake kama pongezi ya ujauzito anaukuza kwa sasa. 

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

‛‛Haaaa ona toy ya kutupeleka clinic, chai huyu toto amekuja na mabakuli, sir God akujaliemume wangu shukran sana,’’ Akothee aliandika katiika mtandao wa kijamii akiambatanisha pamoja na picha inayoonesha gari hilo akiwa jijini Johensberg. 

Aidha, alieka wazi kuwa kilichosalia ni kushuhulikia vibali kutoka pande husika, vibali vitakavyomwezesha kutumia gari hilo nchini Kenya. 

Cha kushangaza zaidi ni jinsi anavyoliita gari hilo kwa lugha ya kimombo (billionairetoy), kwa maana vitu vinavyochezewa na watoto wa mabwenyenye na kuongeza kuwa atakuwa akilitumia gari hilo kwenda katika zahanati kwa ajili ya matibabu maalum ya uja uzito wake pindi atakaporudi nchini.

Ukwasi wake umeendelea kuzua vita baridi  kwa wasanii wenza akiwemo msanii wa kike mzaliwa wa Kenya aliye na makazi yake nchini Qatar anayejulikana kama Sheika.

Shekha ambaye hivi karibuni aliachia wimbo  mpya  Yebede amenadi kuwa atamuonesha Akothee ni nini maana ya kuwa na pesa, baada ya kutuma kipande cha Nyimbo yake mpya.