Wakaazi wa eneo la Kiambu wameraiwa kushirikiana Na maafisa wa polisi katika harakati za kupambana Na uuzaji na unywaji wa pombe haramu.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akizungumza katika ofisi yake, Mkuu wa polisi wa eneo hilo SSP Stephen Ng'etich alisema kuwa uuzaji na unywaji wa pombe hizo ni jambo ambalo limekita mizizi katika kaunti ya Kiambu,na linahitaji suluhu la haraka.

Ngetich alisema kwamba ushirikiano Kati ya wananchi na vitengo mbalimbali vya usalama kutawezesha Kaunti hiyo kukabiliana vilivyo na wale wanaoendeleza biashara hiyo.

Aliongezea kwa kufichua kuwa hivi majuzi idara ya polisi ilifanikiwa kufunga baadhi ya mashimo ambamo uuzaji wa pombe, hususan aina ya chang'aa na muratina unatekelezwa.

Kulingana na Ngetich, baadhi ya maneno yaliyo fanyiwa msako huo ni Banana, Kirigiti na Riabai ambazo ziliibuka bayana katika uraibu huo wa matumizi ya pombe haramu.

Mkuu huyo wa polisi alifafanua kuwa hatua hiyo imefaulu baada ya wakaazi kuhusishwa katika oparesheni ya Mara kwa mara.

Alisema kuwa maafisa wa polisi wanashirikiana Na tume la kukabiliana Na pombe haramu na dawa za kule ya (NACADA) ili kukomesha biashara hiyo ambayo ina madhara makubwa mno katika jamii.

Aidha, afisa huyo alisema msako utaendelezwa hadi vilabini ili kuhakikisha pombe ambazo hazijaidhinishwa Na halmashauri ya ubora wa bidhaa (KEBS) haziuzwi ili kuepusha wakaazi wa Kaunti ya Kiambu kutokana na madhara ambayo yameshuhudiwa mara kwa mara.