Kamishna wa Kaunti ya Mombasa Evans Achoki ametangaza kuanzishwa upya kwa vita dhidi ya pombe haramu na mihadarati katika kaunti hiyo, kufuatia ripoti kuwa pombe hiyo imeanza kuuzwa tena katika eneo hilo.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akizungumza katika kikao na wanahabari siku ya Jumatatu, Achoki alisema kuwa pombe hiyo imeanza kuuzwa tena kwa ajili ya utepeteavu wa maafisa wa polisi na machifu wanaoshirikiana na wauzaji hao.

Aidha, kamishna huyo aliwapa ilani maafisa wa polisi na machifu wanaofanikisha shuguli hiyo kuwa iwapo watapatikana, basi watachukuliwa hatua za kisheri.

Itakumbukwa kuwa hapo awali, Rais Uhuru Kenyatta alikuwa ametangaza vita dhidi ya pombe haramu nchini, shuguli ambayo ilifanikisha kukamatwa kwa walanguzi wengi.