Vituo vya kuandikisha vitambulisho katika kaunti ya Kisii vimeshauriwa kuweka kando vitambulisho ambavyo vimekawia katika vituo hivyo zaidi ya miaka mitatu bila kuchukuliwa ili kupunguza msongamano wa vitambulisho.

Share news tips with us here at Hivisasa

Ushauri huo umetolewa baada ya idadi nyingi ya vitambulisho kukawia kwa vituo hivyo kwa muda mrefu na kupelekea msongamano mkubwa katika afisi hizo.

Akizungumza nasi siku ya Jumatano  mjini Kisii, Mwakilishi wa wadi ya Bogeka eneo bunge la Kitutu Chache Kusini Charles Nyagoto aliomba vituo hivyo kuweka kando vitambulisho hivyo ili kuruhusu uandikishaji wa vingine.

“Hakuna haja kuruhusu vitambulisho kukaa kwa vituo kwa zaidi ya miaka mitatu vitambulisho hivyo viwekwe kando ili uandikishaji mwingine ufanywe upya,” alisema Nyagoto.

Wakati huo huo, Nyagoto aliomba shangazi, mama wakwe na babu wa mayatima kuwakabidhi mayatima vitambulisho vyao ili kutumika kushika vitambulisho kwani imebainika kuwa mayatima wengi hukosa kushika vitambulisho kufuatia ukosefu wa vitambulisho vya wazazi wao .

Aidha, aliwashauri wakaazi wengine ambao wamefikisha miaka 18 kushika vitambulisho kwa wingi ili wakati mwingine wajiandikishe kama wapiga kura na kuchagua viongozi wa maendeleo.