Mbunge wa Garissa Township, Aden Duale aliwasili kaunti ya Garissa siku ya Jumapili alipoongoza hafla ya kuzinduliwa kwa magari mawili ya mabasi katika vituo viwili vya kutoa mafunzo ya dini ya kiislamu.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Vituo hivyo viwili, Khadija Girls Islamic School na Imam Malik Educational Centre, vinatoa mafunzo ya dini ya kiislamu na pia kufunza lugha za kiarabu kando na kutoa mafunzo ya sheria juu ya uislamu. Vituo hivyo viwili vilikuwavikitoa mafuzo bila magari kwa muda wa miaka 23.

Miongoni mwa waliohudhuria katika hafla hiyo ni pamoja na mwalimu mkuu wa Khadija Islamic School, Sheikh Bashir, mwalimu mkuu wa Imam Malik, Sheikh Abdi, viongozi wa dini, wanasiasa na wananchi wa kaunti ya Garissa ambao walijumuika kuona hafla hiyo ya kihistoria ya kuzinduliwa kwa mabasi hayo mawili.

Waliozungumza katika hafla hiyo ni wakuu wawili wa vituo hivyo ambao wametoa shukrani zao za dhati kwa mbunge huyo, Duale na wengine wote walioshirikiana naye katika ufadhili wa ununuzi wa mabasi hayo mawili.

“Tunamshukuru mheshimiwa, Duale kwa kuchangia pakubwa katika ununuzi na ufadhili wa mabasi haya mawili ambayo mnayaona kwa macho yenu siku hii ya leo. Pia tunawashukuru wengine wote ambao wameuchukua asilimia kubwa katika kufanikisha ununuzi wa mabasi haya,” alisema mkuu wa Khadija, Sheikh Ismail.

Mkuu wa Imam, Malik alitoa shukrani zake na kuahidi kuwa wananchi wa kaunti ya Garissa wanasimama kidete kila wakati kufanya kazi na Duale.

“Kwanza tunamshukuru mheshimwa wetu Duale kwa kutuletea magari haya mawili siku hii ya leo na nataka kukuahidi mheshimiwa kuwa sisi kama wananchi wa kaunti ya Garissa tupo tayari kufanya kazi nawe wakati wowote ili tuendelee kufurahia mazuri unayotutendea,” alisema Malik.

Mwishowe, mbunge huyo wa Garissa Township alizungumza katika hafla hiyo akiwarai wananchi wa Garissa kuwa makini watakaposhiriki uchaguzi mkuu ujao.