Baadhi ya vyuo vinavyotoa mafunzo ya matibabu nchini huenda vikafungwa baada ya kukosa vibali vya kuviruhusu kutoa mafunzo hayo.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Akizungumza siku ya Jumatatu mjini Mombasa, Waziri wa Afya Cleopa Mailu alisema kuwa wanafunzi wengi wanahitimu katika vyuo hivyo hawana ujuzi wowote wa kikazi.

Mailu alitaja hali hiyo kuwa hatari zaidi hasa kwa maisha ya Mkenya.

Waziri huyo alisema kuwa Wakenya hulalamikia huduma duni zinazotolewa na baadhi ya wahudumu hao.

Aliongeza kuwa wizara yake itajitahidi katika kupiga vita vyuo na wahudumu bandia nchini.

“Tutahakikisha hivi vyuo havipo tena na vile vilivyopo vimesajiliwa. Kama hilo haliwezekani, itabidi tuvifunge,” alisema Mailu.