Shamrashamra za sherehe ya Krismasi na mwaka mpya wa 2017 zikiwa zimepamba moto, wakaazi Mombasa na Pwani kwa ujumla wametakiwa kuidhinisha sherehe hizo katika njia ya amani.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Kwenye mkao na wanahabara mjini Mombasa, katibu mtendaji wa Baraza la Maimamu na Wahubiri wa Kiislamu nchini (CIPK) sheikh Mohammed Khalifa amemtaka kila mkaazi kudumisha usalama na amani.

Mohammed aidha amewahimiza wakaazi washirikiane vyema na idara ya usalama kwenye Kaunti, na kuripoti visa vyovyote vya uhalifu wanapovishuhudia.

Pia amewataka wazazi kuwa waangalifu kwa watoto wao, ili wasijiingize kwenye makundi ya kigaidi.