Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Kundi moja la watu wanaodai walikuwa wafanyakazi katika shamba moja huko Bahati linalomilikiwa na rais mstaafu Daniel Moi liliandamana hadi Kabarak kudai marupurupu yao siku ya Ijumaa.

Watu hao 27 wakiwemo wakongwe walianza safari yao Ijumaa alfajiri na kutembea miguu hadi kwenye kiingilio cha shamba la Moi wakiapa kuwa watapiga kambi mahala hapo hadi wapate haki yao.

Wakizungumza na mwandishi huyu, wafanyakazi hao walidai walikuwa wakifanya kazi katika shamba la kahawa huko Morop.

Kwa jumla walikuwa wafanyakazi 210 na kuwa hawajalipwa tangu kustaafu kwake na wanasema kwa jumla wanadai shilingi milioni 9 na laki moja.

Juhudi  za kuwasiliana na msemaji wa rais mstaafu Lee Njiru hazikufua dafu.