Familia 100 ambazo zilikuwa zimeachwa bila makaazi kufuatia mafuriko katika eneo la Bangladesh, eneo bunge la Jomvu, zimepata msaada kutoka kwa Shirika la Msalaba Mwekundu, tawi la Mombasa.
Akizungumza baada ya kusambaza bidhaa mbalimbali kama vile chakula kwa familia hizo, mratibu mkuu wa tawi la Mombasa Mohammed Rajab alisema kuwa zaidi ya familia 1000 ziliathirika na kuachwa bila makaazi.
Alisema kwa kuwa vile Bangladesh ni eneo lenye makaazi duni, huenda hali hiyo ikawa mbaya zaidi.
"Tumekuwa tukishirikiana na serikali ya kaunti kutoa bidhaa mbalimbali pamoja na chakula kwa waathiriwa. Pia tumejaribu kuwatafutia waathiriwa makaazi katika familia jirani,” alisema Rajab.
Aliongeza, "Hata hivyo, tunajaribu vile tuwezavyo kuhakikisha kwamba waathiriwa hawa wanapata vyakula pamoja na kuwakinga dhidi ya magonjwa kama vile kipindupindu.