Waathiriwa wa mkasa wa moto katika eneo la Michatha Molo wanaomba usaidizi baada ya moto kuteketeza mali yao yote.
Wakizungumza Alhamisi, waathiriwa hao walisema mali yao yote iliteketezwa kwenye mkasa huo.
“Hatuna chochote na tunauliza wasamaria wema watusaidie hata na chakula ama mavazi. Kila kitu iliungua,” Veronicah Mbuthia alisema.
Moto huo uliteketeza nyumba zaid ya ishirini huku familia takriban arobaini zikiachwa bila makao.
“Nilikuwa shule nikapata nyumba zetu zimechomeka. Kwa sa hii niko na uniform pekee na ninaomba watu watusaidie,” John Kamau, mwanafunzi katika shule ya msingi ya Sulgwita, alisema.
Mbunge wa Molo Jacob Macharia aliwasihi wasamaria wema kutoa msaada wao kwa familia hizo.
Akiongea Alhamisi alipozitembelea familia hizo, Macharia alisema hali hiyo ni ya hadhara.
“Hali ni mbaya sana hapa na yeyote aliye na uwezo asaidie familia hizi,” Macharia alisema.