Waathiriwa wa mkasa wa moto katika eneo la Michatha, eneo mbunge la Molo wamepokea msaada wa mbolea na mbegu kutoka kwa wakfu wa Kuria Kimani.

Share news tips with us here at Hivisasa

Waathiriwa hao 40 waliachwa bila makao baada ya makazi yao kuteketezwa na moto katika eneo la Michatha wiki tatu zilizopita. 

Waathiriwa hao wamefurahishwa na hatua ya wakfu huo kwa kuwakumbuka wakati wa majonzi. 

"Tumefurahi sana kwa kupokea mbegu na mbolea kutoka kwa Kuria Kimani Foundation, sasa tutaeza kupanda wakati huu wa mvua," alisema Josephine Njeri, mkazi mmoja. GWairimu/Hivisasa.com