Wabunge wa Kaunti ya Mombasa wameunga mkono miradi ambayo ilizinduliwa siku ya Jumamosi katika Ruwaza ya 2035 ya kaunti hiyo, kwa kusema kuwa yataboresha maisha ya wakaazi wa Pwani.

Share news tips with us here at Hivisasa

Akiongea katika hafla ya kuzindua ruwaza hiyo, Mbunge wa eneo bunge la Mvita Abduswamad Nassir alisema kuwa miradi hiyo itaboresha sekta mbali mbali ikiwemo sekta za uchumi, afya na utalii.

Kwa upande wake, mbunge wa Kisauni Rashid Bedzimba alisema kuwa kuna haja ya wakaazi wa Pwani kujiepusha na siasa ambazo zitawagawanya kwa misingi ya kikabila au kidini, ili kuhakikisha kuwa miradi hiyo imefaulu.

Mbunge wa Jomvu Badi Twalib alitoa hakikisho kuwa afisi yake kama mbunge itashirikiana kwa ukaribu na viongozi wa kaunti ili kuhakikisha kuwa miradi hiyo imefaulu.