Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Wabunge watano wa Jubilee wamefika mahakamani kufuatia maandamano ya Cord siku ya Jumatatu.

Wabunge hao, Dennis Waweru wa Dagoretti Kusini, Ferdindard Waititu wa Kabete, Alice Ng’ang’a na Kimani Ichungwa walisema Cord inapaswa kuzuia kuhujumu utendakazi wa tume huru.

Aidha, hapo awali, viongozi wa chama cha Cord waliapa kufanya maandamano katika ofisi zote za IEBC ambapo wafuasi wa chama hio waliandamana siku ya Jumatatu mpaka pale wasimamizi wa tume ya IEBC walifunga virago na kuondoka ofisini. Haya yalitokana na kile viongozi hao walichosema kuwa maafisa wakuu wa tume ya IEBC ni wafisadi, wanaegemea upande wa Jubilee, wamehusika katika ufisadi hali maarufu kama 'Chicken Gate' na hawana uwezo wa kusimamia uchaguzi mkuu ujao wa mwaka wa 2017.

Jaji Isaac Lenaola wa mahakama ya juu ameagiza kesi hiyo kama ya dharura na itaskizwa siku ya Ijumaa.