Wabunge wawili kutoka Kaunti ya Mombasa wameapa kumuunga mkono mshirikishi wa kanda ya Pwani Nelson Marwa, kwenye juhudi zake katika vita dhidi ya ulanguzi wa mihadarati.

Share news tips with us here at Hivisasa

Haya yanajiri baada ya Marwa kutoa wito kwa viongozi katika eneo la Pwani kushirikiana naye kukabiliana na janga hilo.

Mbunge wa Nyali Hezron Awiti na mwenzake wa Kaloleni Gunga Mwinga walisema kuwa vijana wengi hawakujitokeza katika zoezi la usajili wa makurutu wa polisi katika kaunti hiyo, kwa kuwa wameathirika na mihadarati.

Wakizungumza mjini Mombasa siku ya Jumatatu, wawili hao walisema kuwa kuna haja ya viongozi wote kujitokeza hadharani ili kufanikisha vita hivyo.

Hapo awali, Marwa alikuwa ametoa madai kuwa huenda kuna viongozi wakuu serikalini na wakuu wa idara ya polisi ambao wanashirikiana na walanguzi wakuu wa mihadarati .