Share news tips with us here at Hivisasa

Wabunge wanne wametakiwa kufika mbele ya tume ya uchaguzi na mipaka IEBC kutoa maelezo kuhusu kuhusika kwao katika uchaguzi wa Malindi na Kericho. 

Nne hao akiwemo seneta wa Kilifi Stewart Madzayo, Agostinho Neto wa Ndhiwa, Ferdinand Waititu wa Kabete na Peter Gitau wa Mwea wametakiwa kuandikisha taarifa na tume hiyo. 

Habari kutoka kwa meneja wa kuendesha uchunguzi katika tume hiyo Chrispine Owiye anasema Madzayo na Neto wametakiwa kufika tarehe 24 mwezi huu huku Waititu na Gitau wakitakiwa kujiwasilisha tarehe 26. 

Wanadai kuhusika na visa vya utoaji hongo miongoni mwa ukiukaji mwingine wa sheria za uchaguzi.

Tayari waziri Charles Keter ameandikisha taarifa.