Chama cha wachapishaji vitabu nchini kimeashiria kusikitishwa kwao dhidi ya uamuzi wa kamati ya bunge kuhusu fedha na bajeti kutozingatia pendekezo lao la kuondoa ushuru unaotolewa vitabu.

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wachapishaji hao ambao mapema mwaka huu waliashiria uwezekano wa kupunguza bei ya vitabu hivyo sasa wamebadili nia na sasa wanataka ushuru unaotolewa vitabu kuondolewa.

Kwa kupitia mwenyekiti wao, David Waweru ongezeko la ushuru unaotolewa vitabu hivyo ina maanisha kuwa wanaosoma watakuwa na vitabu vichache na hivyo basi kutatiza elimu.

Kando na kuwa bei ya juu ya vitabu hivyo kuathiri viwango vya elimu, wachapishaji hao wanasema kuwa biashara yao itaangamizwa kwa kupitia ushuru huo unaotolewa. Sasa wanataka serikali kuondoa ushuru huo unaotolewa vitabu kama ilivyofanya bidhaa zisizo za msingi.

Wito huu unajiri wakati ambapo serikali imetangaza kuwa itaongeza fedha inazotengea shule kwa ajili ya kununua vitabu.