Wafanyikazi wa serikali ya kaunti ya Kisii wamehimizwa kutojiingiza katika siasa na kufanya kazi inayowahusu.

Share news tips with us here at Hivisasa

Kulingana na Mbunge wa eneo la Mugirango Kusini Manson Nyamweya,  idadi kubwa ya wafanyikazi wa kaunti hiyo huudhuria sherehe za mazishi na kupiga siasa jambo ambalo amesema ni kinyume na sheria na kuwaomba kufanya kazi inayowahusu hasa katika kuwahudumia wakaazi wa kaunti hiyo

Akizungumza mjini Kisii Mbunge Nyameya aliomba wafanyikazi hao kufanya kile waliochoajiriwa kufanya na kujitenga na siasa

“Kila ijumaa wasimamizi wa wadi mbalimbali na machifu wanahuduria sherehe za mazishi na kufanya siasa ambazo haziwahusu,” alisema Nyamweya.

“Si vizuri kwa wafanyikazi wa serikali ya kaunti kujiingiza katika siasa maana idadi kubwa ya wafanyikazi wa Kisii kila ijuma huudhuria sherehe za mazishi ma kupiga siasa jambo ambalo ni kinyume na sheria,” aliongeza Nyamweya.

Wakati huo huo, Nyamweya aliomba viongozi wa kaunti ya Kisii kuhakikisha maendeleo yamefanywa inavyostahili kwani wakaazi wanahitaji maendeleo bali sio siasa za kuwapotosha.