Wachongaji vinyago katika eneo bunge la Mugirango Kusini kaunti ya Kisii watafanyiwa uchunguzi kwa kupimwa hali zao ikiwa wana aina yoyote ile za Saratani.

Share news tips with us here at Hivisasa

Hii ni baada ya kusemekana kuwa idadi kubwa ya wachongaji vinyago hao hupoteza maisha yao kupitia Saratani bila kujua sababu.

Akizungumza na wanahabari msimamizi wa chama cha Africa Art Promotion Network eneo la Kisii Elikana Ong’esa alisema chama hicho kitawapima wachonga vinyago hao siku ya jumatano (Kesho) katika eneo la Tabaka.

Ong’esa alisema kuwa zaidi ya wachongaji vinyago 500 watapimwa Saratani ya tumbo, uzazi na zingine nyingi ili kujua hali zao.

“Wachongaji vinyago wamekuwa wakiathirika na aina mbalimbali za Saratani katika eneo hili bila kujua kinachosababisha hayo,” alisema Ong’esa.