Wachumba wanaodaiwa kuhusika katika ulanguzi wa watoto wamefikishwa kizimbani katika Mahakama ya Shanzu, jijini Mombasa.
Margaret Juma Magero na Davidi Ochieng Ometo ambao wanadaiwa kuhusika katika ulanguzi wa watoto watatu watasalia korokoroni kwa muda wa wiki mbili wakisubiri uchunguzi dhidi yao kukamilika.
Hii ni baada ya upande wa mashtaka pamoja na polisi kuomba Hakimu Diana Mochache muda zaidi wa kufanya uchunguzi.
Washukiwa hao wanadaiwa kumuiba Breluin Achieng mwenye umri wa miaka saba katika mtaa wa Maweni eneo la Kisauni, mnamo Machi 18, 2009.
Aidha, wanadaiwa kumuiba Joyce Mbuche mwenye miaka mitano mnamo April 4, 2011 katika eneo la Bamburi na Baby Brian mwenye umri wa mwaka mmoja unusu.