Bunge la Kaunti ya Mombasa limepitisha hoja ya kuondolewa kwa wachuuzi wanaohudumu katika kivuko cha feri cha Likoni.
Mwakilishi wa wadi ya Kadzandani, Mohamed Ndanda, aliyewasilisha hoja hiyo bungeni, alisema kuwa hatua hiyo inanuia kupunguza msongamano wa watu na magari katika kivuko hicho.
Licha ya hoja hiyo kupingwa na baadhi ya wawakilishi wadi, Ndanda alisema kuwa itachangia pakubwa katika kudhibiti visa vya wizi ambavyo vimekuwa vikishuhudiwa kivukoni humo.
Kulingana na Baraka FM, wachuuzi hao wanatakiwa kuondoka kuanzia Alhamisi wiki hii.