Itawabidi wafanyibiasahara waiohamishwa kutoka katikati mwa mji wa Nakuru kuelekea katika kituo cha Nasher kungoja kwa muda zaidi huku serikali ya jimbo ikipanga kuwatengenezea jengo mwafaka kwa biashara zao.
Hii ni kufuatia utawala wa jimbo kuahidi kuwa itawapa wachuuzi hao mahala mbadala na sawa pa kufanyia kazi zao baada ya kuwahamisha kutoka katikati mwa mji.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa maswala ya Ardhi nyumba na mipango maalum katika jimbo la Nakuru Racheal Maina ni kuwa sharti wachuuzi hao wawe wavumilivu akidokeza kuwa serikali ya jimbo inapanga kuwapa vifaa muhimu ikiwemo huduma za maji na usafi wa mazingira
Amesema kuwa serikali ya jimbo inalenga hata kushirikiana na mashirika mengine ili kuwezesha kujengwa kwa mahala mufti pa wachuuzi hao.
Amehoji kuwa hatua ya kusafisha mji wa Nakuru na iliyoanzishwa na gavana wa jimbo Kinuthia Mbugua imeafikia angalau asilimia themanini baada ya wachuuzi zaidi ya elfu mbili wa vyakula vya kutoka shambani kuhamishwa kwenye soko la mkulima liilofunguliwa rasmi mwishoni mwa mwezi jana.
Aidha, amedokeza kuwa waliohamishwa katika eneo la Nasha ni wanaojishugfhulisha na bidhaa zingine kando na vyakula vya shambani.